Wauawa kwa kushindwa kulipa deni la biskuti India
Mtu mmoja na mkewe
kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa,
mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa
deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Polisi
kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana
mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao
kwa kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto
wao.Mfanyi biashara huyo amekamatwa.
Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi la umaskini .
Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii hiyo
No comments:
Post a Comment