Dalili za Martial kuchukizwa kwa namba yake ya jezi kupewa Ibrahimovic
Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambaye kajiunga na Man United msimu huu akitokea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kama mchezaji huru, jina lake linazidi kuingia kwenye headlines baada ya kuchukua jezi namba 9 iliyokuwa inavaliwa na Anthony Martial.
Stori kutoka 101greatgoals.com zinaeleza kuwa Zlatan baada ya kuwasili, viongozi wa Man United walimwambia achague namba ya jezi ambayo angependa kuvaa, Zlatan akachagua namba 9 na viongozi wakakubali pasipo kumuhusisha kwa namna yoyote ile Anthony Martial ambaye alikuwa akiivaa jezi hiyo.
Headlines za Martial kuvuliwa jezi namba 9 na kupewa Zlatan Ibrahimovic bila ridhaa zinapata nguvu kutokana na Anthony Martial kuripotiwa kuunfollow account za Man United za Instagram na twitter, kwa sasa mashabiki wa Man United wanatajwa kuwa na hofu na Martial kuendelea kusalia kikosini kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment