Nusura mwenge wa Olimpiki uibiwe Brazil
Polisi nchini
Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa
Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.
Video
kuhusiana na tukio hilo, inamuonyesha mtu huyo akipigwa mieleka na
walinda usalama, baada ya kuingia katika msafara wa watu na kuelekea
moja kwa moja hadi kwa mtu aliyekuwa na mwenge huyo akiwa na nia ya
kumpokonya.Mtu huyu alinaswa na kuchukuliwa, huku mbio za mamani za mwenge huo zikiendelea muda mfupi baadaye.
Mwenge huo unatazamiwa kufika mjini Rio de Janeiro tarehe 4 mwezi ujao, kabla ya kuanza rasmi kwa mashindano ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment