Saturday, July 23, 2016

MOYES ABEBA MIKOBA YA BIG SAM

Moyes ajiunga na Sunderland

David Moyes apata kazi Sunderland. Atachukua nafasi yake aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Sam Allardyce
David Moyes amebahatika kupata nafasi hiyo baada ya Sam Allardyce kuchaguliwa kuwa msimamizi wa timu ya kitaifa ya Uingereza.
Moyes mwenye umri wa miaka 53, na aliyewahi kuwa meneja wa Manchester United na vilevile Everton amepata mkataba huo mpya wa miaka minne.
Moyes anasema anafurahi kupata kazi na club hiyo kubwa ya Uingereza na anatazamia kwa hamu kurudi tena kufanya kazi katika ligi kuu ya Uingereza Premier League.
Utakumbuka jinsi alivyolazimika kuihama Premier League wakati alipofutwa kazi kutokana na kutopata matokeo mazuri baada ya kuchukua uongozi wa Manchester United kutoka kwa Sir Alex Ferguson aliyekuwa anastaafu baada ya msimu wa mafanikio mazuri wa ushindi wa vikombe kadhaa katika mdaa wa miaka 26 huko Old Trafford.

No comments:

Post a Comment