Kutizama Tv kunaweza kukuua, utafiti

Utafiti uliofanywa
na wanasayansi wa Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na
kutazama vipindi vya televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya
kwani huhusishwa na maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini
kutokuwa sawa.Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.
Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.
Zaidi ya hayo watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.
No comments:
Post a Comment