Mbinu za Leicester City kumzuia Mahrez kujiunga na Arsenal
Mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015/2016 klabu ya Leicester City bado inaendelea kupambana ili kulinda kikosi chake kilichoisaidia kutwaa Ubingwa wa England kisibomolewe, baada ya Leicester City kutwaa taji la England vilabu vingi vikubwa England vinahangahika kuhakikisha vinasajili nyota wa kikosi hiko.
Leicester City wameripotiwa na gazeti la Daily Express kuwa wameamua kumuongezea mshahara winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu hiyo Riyad Mahrez ili asishawishike kujiunga na Arsenal ambao nao wamepanga kumlipa mshahara wa pound 100,000 kwa wiki, hivyo Leicester City wanataka kumlipa mshahara huo ili asiondoke.
Riyad Mahrez ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa PFA, anawindwa na Arsenal na tayari wameripotiwa kuwa wapo tayari kutoa pound milioni 37 kwa Leicester City
ili wampate nyota huyo, ambaye aliwahi kukaririwa kwa wiki za hivi
karibuni akisema kuwa bado hajajua msimamo wake kuhusu kuondoka au la.
No comments:
Post a Comment