Wanyongwa Indonesia kwa dawa za kulevya
Maafisa nchini
Indonesia wamesema hukumu ya kuwanyonga watu wanne kwa kukutwa na hatia
ya makosa ya dawa za kulevya imetekelezwa.
Mwanasheria mkuu wa
serikali nchini humo Noor Rachmad amesema raia watatu wa Nigeria na
Muindonesia mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi katika gereza la kisiwa
cha Nusa Kambangan.Mapema wiki hii mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo amesema watu 14, wengi wao wakiwa ni wageni watanyongwa.
Serikali mbalimbali za kigeni, Makundi ya haki za binadamu na ndugu za watu hao walizitaka Mamlaka nchini Indonesia kuacha kuwaua watu hao.
No comments:
Post a Comment