Kuondoka kwa Uingereza kutoka EU kumeathiri uchumi duniani
Mkutano wa mawaziri
wa fedha wa mataifa ya G20, umemalizika nchini China, huku onyo
likitolewa kuwa, kura ya maoni iliyoifanya Uingereza kujiondoa ndani ya
muungano wa mataifa ya Bara Ulaya, imesababisha hatari kubwa zaidi na
kuyumbisha uchumi wa Dunia.
Mkutano huo wa G20 umesema kwamba kuna
hatari kubwa kuwa, mazungumzo kuhusiana na hatua hiyo ya Uingereza
yakaibua uchungu mwingi.Lakini viongozi hao wakasema kuwa EU imejiandaa ipasavyo kushughulikia tatizo hilo huku wakisema kuwa wana matumaini kubwa kuwa Uingereza sharti iendelee kuwa mshirikamkubwa wa EU.
No comments:
Post a Comment