Man United kujifua China
Kikosi cha
Mashetani wekundu Manchester united kimeenda China katika kujiandaa na
msimu mpya.Wakiwa huko China, United watacheza mechi mbili ya kwanza
watacheza na klabu ya Borussia Dortmund mjini Shanghai, siku ya ijumaa
na kisha jumatatu watacheza na Manchester Man City,jijini Beijing.
Jumla
ya wachezaji 25 ndio wako kwenye msafara wa timu hiyo wakiwamo nyota
wapya Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan pamoja na Chipukizi tisa toka
chuo cha soka cha Man United, huku wachezaji wengine walioshiriki
michuano ya ulaya wakiachwa kuendelea kupumzika.Man United wanakwenda katika ziara hiyo wakiwa chini ya mkufunzi Jose Mourhino mwenye kibarua cha kurudisha thamani ya timu hiyo .
BBC
No comments:
Post a Comment