Chelsea sasa wapo radhi kutoa zaidi ya Tsh Bilioni 190 kwa ajili ya Lukaku
Dirisha la usajili la msimu huu kwa
vilabu vya soka barani Ulaya linazidi kuvutia zaidi, hii inatokana na
vilabu vingi sasa kutaka kuwarudisha katika timu zao wachezaji wao wa
zamani kwa gharama kubwa wakati waliwaacha waondoke kirahisi misimu
kadhaa iliyopita.
Man United wanataka kuvunja rekodi ya usajili kwa kumridisha Pogba, Real Madrid wamemrudisha Morata kikosini, Borussia Dortmund tayari wamemrudisha Mario katika kikosi chao, sasa Chelsea inajiandaa kutoa euro milioni 80 kwa ajili ya kuishawish Everton imuachie mchezaji wao wa zamani Romelu Lukaku arejee Stamford Bridge.
Mwandishi Ivan Zazzaroni wa gazeti la dello Sport ameandika katika gazeti kuwa Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kwa ajili ya kumrudisha mshambuliaji wao Romelu Lukaku aliyeondoka Stamford Bridge 2014, Lukaku ameondoka Chelsea akiwa kacheza mechi 10 katika kipindi cha miaka mitatu alipojiunga nayo akitokea Anderlecht.
millardayo
No comments:
Post a Comment