Wednesday, July 20, 2016

POGBA AWEKA RECODI YA DUNIA

Man United wamekubali kumsajili Pogba kwa rekodi ya dunia

Siku moja baada ya klabu ya Man United kuripotiwa kutoa pound milioni 90 kwa klabu ya Juventus ya Italia ili kuishawishi iweze kumuachia mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba ajiunge na klabu ya Man United na ofa hiyo kukataliwa.
Juventus wapo tayari kumuachia Paul Pogba arudi Man United ila kwa uhamisho wa rekodi ya dunia na sio pound milioni 85 au 90, usiku wa leo July 20 2016 Man United wameripotiwa na The Sun kuwa tayari kulipa pound milioni 105 ambazo ni zaidi ya bilioni 300 za kitanzania ili kumsajili Pogba.
pog-691404
Wakala wa staa huyo Mino Raiola anatajwa kuendelea na mazungumzo ya karibu na Man United pamoja na Juventus, kama Pogba akikamilisha usajili huo kwa ada hiyo atakuwa mchezaji ghali zaidi duniani na kuwapiku Gareth Bale na Cristiano Ronaldo, Pogba atasaini Man United miaka mitano na itakuwa ni mara yake ya pili kucheza Man United toka aondoke 2012.

No comments:

Post a Comment