Thursday, July 21, 2016

LIVERPOOL YAFANYA KUFURU USAJILI

Sahau kuhusu Klavan Liverpool wamesajili staa mpya kwa zaidi ya Tsh bilioni 70

Bado siku zinahesabika kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu England kwa msimu wa 2016/2017, vilabu karibia vyote vinapigana vikumbo kuwania saini za mastaa wapya katika vikosi vyao, klabu ya Liverpool leo July 21 2016 imefanikiwa kukamilisha usajili wa staa mpya kutoka Newcastle United.
Liverpool imekamilisha usajili wa Georginio Wijnaldum kutoka Newcastle United, ikiwa ni siku moja imepita toka wakamilishe usajili wa beki wa kimataifa wa Estonia Ragnar Klavan kutokea FC Augsburg ya UjerumaniGeorginio Wijnaldum alitumia account yake ya twitter kutangaza safari yake ya Liverpool.
2D89B6C100000578-3278185-image-a-152_1445188064052
Sky Sports wameripoti kuwa Georginio Wijnaldum amesajiliwa kwa pound milion 25 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 70, Wijnaldum alisajiliwa na Newcastle United kwa pound milioni 14.5 akitokea PSV na aliifungia magoli 11 msimu uliopita licha ya kushuka daraja.

No comments:

Post a Comment