Thursday, July 21, 2016

HARUFU YA KUKU HUZUIA MALARIA, UTAFITI

Harufu ya kuku inazuia Malaria

Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,, Fuga kuku !
Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.
Watafiti nchini Ethiopia na Sweden wamegundua kuwa mbu wanaobeba vimelea visababishavyo ugonjwa wa Malaria huwa wanafanya kila wawezalo kukaa mbali na ndege huyo anayefugwa majumbani.
Moja kati ya majaribio katika utafiti huo ilijumuisha kumweka kuku aliyehai karibu na mtu aliyelala chini ya chandarua kinachozuia kuumwa na mbu.
Mwaka uliopita watu laki nne 400,000 walikufa kutokana na ugonjwa wa malaria barani Afrika, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Japo idadi na visa vya maambukizi ya Malaria vinaendelea kushuka, wataalamu wanaendelea kutafuta mbinu bora zaidi ya kuangamiza kabisa ugonjwa huo.
Vimelea vya malaria hujificha ndani ya maini kabla ya kuambukizwa kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwengine kupitia kwa mbu wa kike anayefyonza damu.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Malaria umebaini kuwa mbu hunusa harfu ya mnyama kabla ya kumuuma.
Hata hivyo hawajui nini katika harufu ya kuku inawapa kinyaa mbu .
Katika hatua ya pili ya utafiti huo sasa, watafiti hao wanalenga viungo vya harufu ya kuku ilikuunda kinga dhabiti dhidi ya mbu hao wanaoambukiza malaria.
Habtie Tekie kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa Ethiopia anasema kuwa mipango inaendelea na huenda majaribio yakatekelezwa karibuni.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sweden walihusika katika utafiti huu.
Iligundulika kuwa idadi ya mbu ilipungua kwa asilimia kubwa sana mahala popote ambapo viungo vya kuku vilitumika ima ni manyoya ama sehemu zingine za kuku.
Wanasayansi wanasema kuwa kuna haja ya kuendelea kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na mbu kwani hata sasa mbu wanaonesha dalili ya kuwa sugu dhidi ya madawa yaliyoko sasa.

No comments:

Post a Comment