Clinton amteua Tim Kaine kuwa mgombea mwenza
Bi Hillary Clinton (Kushoto) akiwa na Tim Kaine
Bi Clinton alitangaza uteuzi huo kupitia akaunti yake ya Twitter
akimtaja mgombea mwenza huyo kuwa ni mfuasi mkubwa wa makubaliano huru
ya biashara na anatarajia kumtambulisha rasmi leo katika mkutano wa
hadhara huko Miami.
Kaine ambaye anaongea kihispania vizuri anatarajia kuwavutia wapiga kura
wamarekani wenye asili ya Uhispania kundi ambalo ni kubwa katika
chaguzi za Marekani.
No comments:
Post a Comment