Thursday, July 28, 2016

MSIMU WA MAVUNO


Wakulima shamba la mbunga Chumvini Tanga, wakivuna mpunga aina ya Barmata, wakulimahao wamedai msimu huu wa mavuno umekuwa haba kutokana na mpunga wao kushambuliwa na wadudu na magugu..
Mpunga ni moja ya kilimo kikuu Tanga ambacho kimekuwa kikitegemewa na wakazi wengi wa Tanga ambapo baadhi ya Mikoa jirani huja kwa kununua mpunga.
Hata hivyo baadhi ya wakulima wamekuwa wakilalamika kukosa utaalamu wa Maofisa Ugani na kupelekea kuvuna mazao kidogo.

 Mkulima wa mpunga shamba la Chumvini Tanga, Ngwali Mbwana akionyesha mpunga aina ya Barmata aliovuna katika shamba lake na kudai kuwa msimu huu wa mavuno umekuwa haba kutokana na mpunga wao kushambuliwa na wadudu na magugu.







 Wajasiriamali wanawake kijiji cha Ngome Tanga, wakivuna mpunga katika shamba la Chumvini na kupeleka katika masoko

No comments:

Post a Comment