Tangakumekuchablog
Tanga, SHULE ya
Msingi Mkwakwani halmashauri ya jiji la Tanga, yenye wanafunzi 1,223
inakabiliwa na uhaba wa madawati na wanafunzi kulazimika kusomea chini.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Aidan
Kassian akizungumza na waandishi wa
habari waliofika kutaka kujua changamoto
inayoikabili shule hiyo baada kuwa ya mchanganyiko na shule ya Bombo kufuatia majengo
yake kuwa chakavu na wananfunzi kulazimika kuhamia shuleni hapo.
Alisema kuna changamoto nyingi
ikiwemo wingi wa wanafunzi kurundikana darasa moja na wengine kulazimika kukaa chini
kufuatia uhaba wa madawati na kuwa kero kwa wanafunzi.
“Shule yangu changamoto kubwa ni
uhaba wa madawati na madarasa baada ya shule ya bombo kuhamia hapa kufuatia
majengo yao kuwa hatarishi, madarasani kuna mrundikano wa wanafunzi” alisema
Kassian na kuongeza
“Kwa wingi huu wa wanafunzi napatwa
na kitisho cha kuzuka kwa magonjwa ya miripiko kwani tuko na matundu ya kumi na
nne ambapo saba ni ya wanaume na saba kwa
wanawake” alisema
Alisema kuna baadhi ya madarasa
wamekuwa wakilazimika kuwaweka wanafunzi 160 kwa darsa moja jambo ambalo
limekuwa kero kubwa kwa mwalimu kufundisha na kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
ya shule, Sauda Singo, alisema zinahitajika jitihada za kuhakikisha changamoto
za madawati na vyoo kupatiwa ufumbuzi wa mara moja ukiwemo wa uzio wa shule.
Alisema shule hiyo haina uzio jambo
ambalo linawafanya wanafunzi kutoka na kuingia bila mpangilo na kushindwa kuwadhibiti
na ulinzi wakati wa usiku.
“Shule haina uzio jambo
linalowapelekea wanafunzi kuingia na kutoka bila mpangilio pamoja na kushindwa
kuwatambua na kuwadhibiti “ alisema Singo
Alisema ili kuendana na kasi ya
elimu amewaomba wadau wa elimu kutoa msaada kwa shule hiyo kipindi hiki cha
mchanganyiko wa shule mbili kufuatia ya Bombo kuwa chakavu na kuhatarisha
usalama wa wanafunzi darasani.
Mwisho
Wanafunzi wa shule ya awali ya
Mkwakwani halmashauri ya jiji la Tanga Tanga, wakiandika chini kufuatia uhaba
wa madawati shuleni hapo. Darasa hilo liko na wanafunzi 161.
Wanafunzi wa shule ya Msingi darsa la 4 Mkwakwani halmashauri ya jiji la Tanga, wakisomea chini kutokana na uhaba wa madawati shuleni hapo, shule ni mchanganyiko na shule ya msingi ya Darajani baada ya wanafunzi kuhamishwa kutokana na uchakavu. Darasa hilo liko na wanafunzi 163 ambao husoma kila siku.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment