Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA Msaidizi wa African Sports ya
Tanga inayoshiriki ligi daraja kwanza Tanzania Bara, Ali Mdoe, amesema kipigo
walichokipata kutoka kwa Polisi Dar ni kutokana na wingi wa majeruhi na uchovu
wa wachezaji.
Akizungumza mara baada ya kumalizika pambano lao na maafande
hao kutoka Dar juzi, Mdoe alisema timu yake inapambana na majeruhi ambapo
mlinda mlango namna moja hadi washambuliaji.
Alisema mbali ya kuonyesha kandanda safi lakini wenzao
walikuwa wakizitumia nafasi ambazo wamekuwa wakizipata na kipindi cha pili
walikaba mwanzo mwisho na kushindwa kupata upenyo wa kulifikia lango lao.
“Kikosi chengu kinasumbuliwa na majeruhi na kama
ilivyoonekana mlinda mlango nambari moja hakuwepo, viungo na washambuliaji
muhimu pia hawakuwemo nah ii ndio siri ya wenzetu kutufunga” alisema Mdoe na
kuongeza
“Tunaingia katika mzunguko wa pili w aligi tukiwa na pointi
nne kibindoni ambayo hazifurahishi, tunarudi kambini kuzitafakari na nini
tuafanye ili kushinda mfululizo mechi zilizoko mbele yetu” alisema
Mdoe aliwataka wachezaji wake kujituma kwa nguvu zote kwa
kufanya mazoezi pumzi na viungo mfululizo kuhakikisha mzunguko wa pili wa ligi
wanafanya vizuri na washabiki wa timu hiyo kuwa na imani ya ushindi.
Kwa upande wake Kocha wa Polisi Dar , Ngero Njanyaba, alisema
ushindi wa mabao mawili ugenini umewaweka katika nafasi nzuri na kuwapa
changamoto wachezaji wake kujiamini.
Alisema kucheza ugenini na kunyakua pointi tatu muhimu ni
faraja ambayo inakupa nguvu ya kuendeleza ushindi kwa kila mchezo ambao uko
mbele yako .
‘Africansports ni timu nzuri na ilicheza vizuri kipindi cha
pili lakini tulitambua kuwa wataingia kama mbogo aliejeruhiwa jambo ambalo
lilinifanya kuwabadilisha beki na kuongeza viungo” alisema Njanyaba
Alisema kwa ushindi huo wa ugenini anawapa pongezi wachezaji
wake kwa kucheza kwa bidii na kuzilinda pointi tatu muhimu Mkwakwani hivyo kwa
sasa mawazo yao ni mchezo ambao uko mbeleni.
Mwisho
Wachezaji wa Polisi Dar wakitoka uwanjani kwa furaha baada ya kuifunga African sports
No comments:
Post a Comment