Samaki anayejiponya uti wa mgongo
Watafiti nchini
Marekani wamesema wamebaini aina fulani ya samaki anayeweza kuzalisha
upya uti wake wa mgongo unapovunjika wanaweza kusaidia kubuni matibabu
yatakayoweza kuwasaidia watu waliopooza kutembea tena.
Wanasayansi
wamegundua kuwa samaki huyo ajulikanaye kama Zebra Fish anapovunjika
uti wa mgongo, huzalisha sehemu nyingine ya uti wa mgongo na kuunganisha
kama daraja sehemu zilizokatika kwa kutumia aina ya protini mwilini
mwake.Wanadamu wanayo aina hiyo ya protini inayoweza kuzalisha mifupa lakini haifanyi kazi sawa na ile ya samaki huyo.
Aina hiyo ya protini kwenye binadamu inafanana kwa asilimia 90 na aina hiyo kwenye samaki hao.
BBC
No comments:
Post a Comment