Sunday, February 22, 2015

KAMA ULIPITWA NA MAGAZETI YA LEO, HEBU PERUZI HABARI TANO KUBWA HAPA

Na wewe uzipate hizi stori kubwa tano TZ, zinatoka kurasa za MAGAZETINI February 22

nuz
MTANZANIA
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka amesema hataki kuzungumzia sakata la kufukuzwa kwake wala mwenendo wake nje ya Utumishi wa Serikali na kwa yeyote anayetakakumzungumzia aendelee, hawezi kumzuia.
Kwa sasa napumzika, chochote tutakachojadili hakiwezi kubadili ukweli wa mambo naomba niwe ‘off limit’, siwezi kuzungumza kitu chochote kwa sasa.. Huu ni wakati wa watu kusema acha waseme siwezi kuwazuia kwa sababu ni wakati wao“– Prof. Tibaijuka.
Wakati akiamua kukaa kimya kumekuwa na taarifa kwamba anajiandaa na kujinusuru na adhabu ya kuvuliwa nyadhfa zake ndani ya CCM pamoja na kulipua bomu la jinsi alivyoombwa kumshawishi Rugemalila kukubali kuuza hisa zake kwa mmiliki wa IPTL.
MTANZANIA
Ikulu imesema mwanasiasa Paul Makonda anayetuhumiwa kwa utovu wa nidhamu ni kijana mzuri anayefaa kuteuiwa kushika nafasi ya Mkuu wa Wilaya, kwa wale wanaopinga wanapiga porojo.
Nani anapingwa, ni wangapi wanapingwa? Si huyu mmoja tu (Makonda). Ngoja nikueleze, Katiba ya nchi yetu ma-DC wanateuliwa na Rais na baada ya kujiridhisha na kushauriwa juu ya mtu anayemteua, sikumbuki ni lini watu wamelalamikia uteuzi wa ma-DC zaidi ya kipindi hiki“– Salvatory Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.
Uteuzi wa Rais siyo zawadi, no! siyo zawadi, watu waelewe hili. Rais anatafuta watu wa kuisaidia nchi kuanzia katika Wilaya, Mikoa na siyo kumridhisha kila mtu, kwahiyo wanaosema wana haki yao ya kusema“– Rweyemamu.
Kuhusu mijadala inayoendelea kupinga uteuzi wa Makonda amesema haiishtui Ikulu kwa kuwa Makonda ana maadili mema, tukio linalomweka kwenye katika kundi la vijana watovu wa nidhamu hakulitenda.
NIPASHE
Lugha ya Kikorea ambayo inaandikwa kwenye dawa za tiba asilia kutoka Korea Kaskazini ambazo zimeelezewa kuweka afya za Watanzania hatarini imesemekana ni lugha ngumu kwa watu kuielewa tofauti na utaratibu ambao unatakiwa wa kuweka lugha ya sehemu husika.
Uchunguzi wa Gazeti la NIPASHE umeonesha Waganga wa Kienyeji kutoka Korea wamekuwa wakitoa huduma kwa kutumia vifaa vya umeme kutetemesha mwili ambavyo inasemekana havina manufaa yoyote zaidi ya kuathiri vimelea vya magonjwa na kusababisha athari za muda mrefu.
Kutoelewana kwa lugha kati ya mgonjwa na na watoa huduma kumetajwa kuwa moja ya sababu zinazosababisha kutolewa kwa dawa ambazo haziendani na ugonjwa husika.
Miongoni mwa vituo vinavyotoa huduma hizo vimeshtushwa na taarifa hizo huku wakikataa kutaja majina, nyadhifa na kupigwa picha.
HABARI LEO
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amepiga marufuku ukarabati wa Maabara za zamani za shule za Sekondari na kuagiza kuwa ni lazima zijengwe mpya kama ambavyo Serikali ilielekeza.
Mmefanya ukarabati kwenye jengo ambalo limekuwepo zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kuna chumba nimekuta ni kidogo mno sababu hakiendani na maelekezo ya sasa.. Chumba kimoja kimepasuka ukuta, hapana!.. Huu ukarabati uliofanywa ni kinyume na maelekezo ya Serikali ya kutaka zijengwe maabara mpya ili zidumu miaka mingi kidogo..“– alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa Iringa.
Waziri Mkuu pia alikataa kuahidi mchango wake kwenye ukarabati huo na kuwaeleza kuwa hiyo itakuwa ni upotevu wa fedha, ila yuko tayari kuchangia ujenzi wa jengo jipya.
NIPASHE
Ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa askari wa JKT waliokosa ajira, George Mgoba kueleza jinsi alivyotekwa na kuteswa, wenzake wametaka uchunguzi huru ufanyike kubaini sindano aliyochomwa kama ilikuwa na sumu huku ndugu zake wakilazimika kumhamishia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Makamu Mwenyekiti wa vijana hao, Parali Kiwango amesema wanachotaka kujua ni sumu aliyochomwa mwenzao na hatua zitakazochukuliwa na kwa sasa wanasimamia matibabu ya mwenzao na kuchagua sehemu ya kumfanyia uchunguzi ili kuzuia serikali kuficha baadhi ya ripoti.
Tunachotaka sisi kama viongozi na polisi tushirikiane kuteua hospitali huru ya kuchunguza afya ya mwenzetu, lakini polisi wamekuwa wakituzuia kushiriki kwenye hilo tunaona kunausiri unaoendelea,”– Parali Kiwango.
Akielezea kuhusu hali ya Mgoba, alisema bado siyo nzuri na kwamba tayari alishachukuliwa sampuli mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi.
Tumeambiwa vipimo vinafanywa nje ya Muhimbili, lakini hatujui ni hospitali ipi, ubinafsi huu tulianza kuuona kutoka Hospitali ya Tumbi tulipotaka kumchukua walitukatalia walitugomea na wao kutudanganya wanampeleka hospitali kumbe walimleta kituo cha Polisi Kati kwa mahojiano zaidi,”– alisema Parali Kiwango na kuongeza kuwa leo wamepanga kutoa tamko rasmi kuhusu sakata hilo.
Kiwango amesema maisha yao yapo hatarini baada ya kuwepo watu wanaowafuatilia majumbani na kila wanapokwenda.
Naibu Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika alisema mara zote jeshi la polisi limekuwa likisema uongo dhidi ya matukio ya utekaji na uteswaji wa watu na kukumbushia kuhusu ishu ya Dk. Ulimboka, kutekwa na kushambuliwa kwa Absalom Kibanda, ambayo amesema hadi sasa Serikali imekuwa na kigugumizi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameliambia gazeti la NIPASHE kuwa upelelezi wa tukio hilo utahusisha mkoa wake wa kipolisi na mkoa wa Pwani.
Tumeanza uchunguzi na mara utakapokamilika basi tutaueleza Umma, tunaomba utulivu wakati hili likiendelea,”– Kamanda Kova.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment