Monday, February 23, 2015

AKODI GARI LA MATANGAZO KUFUTA UDUGU

JAMAA AKODI GARI ZA MATANGAZO KUFUTA UDUGU
largeMwanaume mmoja aliyekodi gari la matangazo ili kwenda kuvua undugu mwanamke ambaye alikuwa ndugu yake wa hiari, msafara ambao ulianzia Vingunguti hadi Kitunda.
Mwanamke huyo ambaye hakujua chochote kinachoendelea aliambiwa kuwa anakuja kufanyiwa usafi siku moja kabla ya sherehe yake ya kuzaliwa, walipofika nyumbani kulikuwa na burudani ya muziki na baadaye MC alitangaza mwanamke huyo asogee mbele halafu akatuzwa elfu 80.
Baada dada huyo kutuzwa MC Nick alitangaza kuwa alikuja kurudisha kiasi hicho cha fedha alichotuzwa na mwanamke huyo anayeitwa July, kutokana na maneno ya uongo yaliyosambaa mtaani baada ya mwanamke huyo kumtunza kiasi kama hicho kwenye siku yake ya kuzaliwa na hivyo aliamua kuzirudisha na kusema undugu wao unaishia hapo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment