Friday, February 27, 2015

WANANDOA WALIOKUFA MUDA NA SAA MOJA

Safari ya mwisho kwa wanandoa hawa wakiwa wameshikana mikono.

shakingTumeshuhudia ndoa nyingi zikifungwa siku hizi lakini hazidumu, chache ambazo zimedumu ama zinadumu kwa muda mrefu.
Wanandoa hawa kutoka California, Marekani ambao walioana miaka 67 liyopita walikufa kwa kupishana saa chache wakiwa wameshikana mikono.
Floyd Hartwig mwenye miaka 90 na mkewe Violet mwenye miaka 89 wamefariki February 11 mwaka huu wakiwa nyumbani kwao baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Family photo of Floyd Hartwig and wife Violet who died hours apart while holding hands
Floyd Hartwig akiwa na mkewe Violet wakati wa ujana wao
“Walikua wakifurahia maisha yao kila siku,walipendana sana,walifanya kazi kwa kujituma na kuheshiamiana sana“alisema mmoja wa watoto wao Donna Scharton.
Kutokana na ukaribu wao familia hiyo baada ya kuwauguza kwa muda mrefu huku wakiwa wamewatengenisha vitanda baadaye waliamua kuwaweka pamoja.
Floyd ambaye alikua wa kwanza kufariki baada ya kusumbuliwa na kansa ya utumbo huku akiwa amemshika mkewe mkono na baada ya saa tano mkewe naye alifariki na kujikuta wote wakiwa wameshikana mikono pamoja.
Hakuna story itakayokupita , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment