Thursday, February 26, 2015

SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO,TZ

Kutoka MAGAZETINI leo February 27, 2015 hizi ni Stori 8 kubwa zilizopewa HEADLINE. Zinaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Candle Education Centre(Wataalamu wa Elimu kuanzia kidato cha 1 hadi V1, 0715 772746,Tanga

cofeMWANANCHI
Wakati Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka jana alitumia dakika 415 (takribani saa 7) akibishana katika mpambano mkali wa kisheria kuhusika kwake katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge aliamua kutimkia Mahakama Kuu kukwepa kuhojiwa na Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Jana, mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Hamisi Msumi alitoa uamuzi kuhusu pingamizi la Chenge aliyetaka baraza hilo lisisikilize shtaka lake la kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
Hata hivyo, Chenge alikwamisha kwa mara ya pili baada ya kuomba kwenda Mahakama Kuu kutafuta tafsiri iwapo baraza hilo linaweza kusikiliza shauri lake kinyume na amri ya mahakama iliyoagiza lisijadilie na taasisi kwa kuwa kuna kesi kadhaa mahakamani zinazohusiana nalo.
Profesa Tibaijuka na Chenge kila mmoja aliingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye akaunti zao binafsi kutoka kwa mkurugenzi wa VIP Engineering iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa za kampuni ya Independent Power Solution Limited (IPTL).
Baraza hilo, linasikiliza mashauri hayo kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 katika vipengele vya matumizi mabaya ya madaraka na sakata la escrow.
NIPASHE
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amekoleza moto wa sakata la mabilioni ya fedha zinazodaiwa kufichwa benki nchini Uswisi kwa kuzitaka mamlaka zinazochunguza, kuzitaifisha ili zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.
Nchemba alitoa wito huo  jana wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Kituo cha Redio One nchini.
“Kuficha fedha nje ni uhujumu uchumi kwani fedha yeyote iliyofichwa nje ni lazima itakuwa imepatikana kwa njia zisizokuwa halali na mtu wa namna hiyo anatakiwa fedha zake zitaifishwe zisaidie katika maendeleo na kusomesha yatima,”:-Nchemba.
Alisema takwimu zinaoonyesha kuwa fedha zinazoombwa katika mataifa yaliyoendelea duniani  zinazotoroshwa na kufichwa nje kutokana na rushwa au matumizi mabaya ya madaraka hali inayodidimiza maendeleo ya nchi.
Alisema serikali ilishaanza kuchukua hatua kwa kushirikiana na vyombo vya nje kuchunguza watu walioficha fedha nje ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Tuna chombo kinachojulikana kama Financial Intelligence Unit (Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu), ambacho kinashirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na vyombo vingine vya usalama kudhibiti masuala kama hayo,”alisema.
Aliyataka mataifa makubwa yasisubiri tu kufuatilia fedha za misaada yanayotoa katika nchi za Afrika badala yake yasaidie kuchunguza ili kuunga mkono nchi zinazoendelea kukabiliana na watu wanaoficha fedha nje.
NIPASHE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,jana iligeuka mithili ya uwanja wa sinema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwafutia mashitaka watu 30 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutimua mbio na kutoweka eneo la mahakama hiyo.
Kitendo hicho kiliwafanya wafuasi hao wanusurike kuunganishwa katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mahakama hiyo.
Tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mawakili wa Serikali, Joseph Maugo na Mwanaamina Kombakono, kudai kuwa DPP amewasilisha hati ya kuwafutia kesi washtakiwa na hivyo, hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Alidai DPP analiondoa shauri hilo chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Sheria za Makosa ya Jinai (CPA).
Hakimu Mchauru alisema kwa kuwa DPP ameona hana nia ya kuendelea kuwashitaki, mahakama yake haina sababu ya kuendeleaa kuwashikilia washtakiwa, hivyo inawaachia huru.
Baada ya washtakiwa hao kuachiwa huru walitoka eneo la mahakama na kutimua mbio wakiwa sambamba na wadhamini wao.
Saa 5:10 asubuhi, mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mchauru, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba alipanda kizimbani kusikiliza kesi yake.
Jopo la mawakili wa serikali liliomba mahakama kubadilisha hati ya mashitaka na kuwaunganisha wafuasi 30 pamoja na Profesa Lipumba, wakati huo wakiwa wamekwishaondoka katika eneo la mahakama na kutawanyika.
NIPASHE
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amesema tukio la kufanyiwa fujo aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, limempa umaarufu mkubwa na kumuwezesha kupata nafasi hiyo.
Alisema hayo alipohojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam, ambacho mtangazaji alitaka kujua kumekuwa na mazungumzo mengi kwenye mitandao ya kijamii ikielezea na kukosoa uteuzi wake.
Makonda, ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka kundi la watu wenye malengo yanayofanana, alisema tukio hilo halijaathiri masuala yake ya kisiasa, badala yake limezidi kumpaisha.
Kila tukio linaweza kuwa na mtazamo wa aina mbili negative (chanya) na positive (hasi). Mimi bahati mbaya najua kila tukio. Chochote kinachokuja mbele yangu ni sehemu ya kunisaidia mimi kusonga mbele,”:-Makonda.
Alisema tukio la kufanyiwa fujo Jaji Warioba, lilimfanya kila mtu ndani na nje kumuulizia ili kumjua yeye (Makonda).
Baada ya tukio lile, Tanzania hii na nje kila mtu alitaka kujua Paul Makonda ni nani, katokea wapi, anafanya nini, ni mtu wa namna gani, ana umbo gani? Lugha hiyo imesababisha mimi anione na kunitafuta na kupitia hivyo imempelekea kunifahamu na mimi nimemjua,” alisema Makonda.
Aliongeza: “Wale waliokuja kugundua ni propaganda za kitoto wanabaki tutakusaidia, wewe ni rafiki yetu, nimepata marafiki na napokea mawazo mengine.”
Novemba 3, mwaka huu, Jaji Warioba alifanyiwa fujo zilizosababisha kuvunjika kwa kongamano la kujadili mambo ya msingi ya kuangaliwa katika katiba inayopendekezwa, lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na wazungumzaji wakuu walikuwa ni waliokuwa wajumbe wa tume hiyo.
MTANZANIA
Mwanaume mmoja Deogratius Mrosso  mkazi wa Kitongozji cha Mreyai Mkoa wa Kilimanjaro amemuaa mkewe na kumzika kwenye zizi la Ng’ombe.
Kamanda wa polisi Godfrey Kamwela alisema alisema tukio hilo lilitokea saa 11 ambapo mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Jenipher Peter alikutwa amekufa kwenye zizi la ng’ombe na kwama mwili wake uligundulika ukiwa umefukiwa na udongo baada ya muuaji kumpigia jirani yake na kumtaarifu juu ya tukio hilo.
Baada ya jirani huyo kupata taarifa hiyo, alitoa taarifa kwa uongozi wa kitongoji na viongozi walipofika walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa umefukiwa na udongo, na walipofukua walimkuta ana majeraha  mbalimbali puani na kichwani-Kamwela.
Alisema muuaji huyo inaonekana alishawahi kutumikia kifungo katika gereza la mahabusu la Ubukoni baada ya kupatikana na hatia ya kuuza bangi la gongo.
Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo kwa kuwa baada ya mauaji hayo alitoroka.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment