Friday, February 27, 2015

MTOTO WA MIAKA 10 AJIUGA NA CHUO KIKUU UINGEREZA

Huyu mtoto yupo Chuo kikuu, umri wake umemfanya awe kwenye HEADLINES…

estaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaKipaji cha mtoto huanza kuonekana taratibu wakati anaendelea kukua, mara nyingi wazazi huwa wanakua wa kwanza mzazi ndio wakati wa kutambua mwanae anataka nini kwa maisha yake ya baadaye lakini kipaji cha mtoto Esther Okade kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja.
Unaweza usiamini lakini huu ni ukweli, Esther ambaye ana umri wa miaka 10 amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha Uingereza miezi mitatu iliyopita akisomea shahada ya hesabu.
Eshte
Mtoto huyo ambaye anatokea katika mji wa Walsaw uliopo Midlands, Uingereza sio mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake, mdogo wake wa kiume mwenye miaka sita anasoma masomo ya kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
MOM
Esther akiwa na mama yake mzazi, Ife
Pamoja na Esther kudahiliwa miezi mitatu iliyopita ameonekana kufanya vizuri kuzidi wenzake darasani.
Mama yake Esther aitwaye Ife anasema kitendo cha mwanae kujiunga chuo kikuu kilikuwa la kushangaza kutokana na umri wake kuwa mdogo lakini mwenyewe alijiamini na kuona anaweza.
YOUNG
Esther akiwa na mdogo wake Isaya
Tangu akiwa na miaka saba alikuwa na shauku ya kujiunga na chuo kikuu ili atimize ndoto zake, alikua na kipaji cha aina yake darasani na baada ya miaka mitatu aliuliza tena ikabidi tumpeleke ili kuona kama kweli atamudu“– amenukuliwa Ife, mama wa Esther.
Historia inaonyesha kuwa Esther si wa kwanza kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri mdogo, mwaka 1981 mtoto aitwaye Ruth Lawrance alijiunga na chuo kikuu cha Oxford na kuhitimu mwaka 1985.
Hutopitwa na habari yoyote na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment