Wednesday, February 25, 2015

MWENGINE UINGEREZA AFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUFANYA UCHAFU AKIWA KAZINI

Ile picha ya askari kupigana mabusu Bongo iliteka HEADLINES! iko hii mpya toka Uingereza…

poliseUnakumbuka ile Stori ya askari Asuma Mpaji na Veronica Nazaremo kufukuzwa kazi Mkoani Kagera baada ya picha zao kusambaa mitandaoni wakionekana kupigana mabusu? safari hii nakuletea tena stori inayofanana na hiyo ambayo imetokea Nchini Uingereza.
Polisi wa nchi hiyo Uingereza waliamua kumshtaki mwenzao baada ya kufanya kitendo cha kudhalilisha jeshi  hiyo kwa kufanya tendo la ndoa tena mbele za watu akiwa na sare za kazi.
Kitendo hicho kimemfanya kufukuzwa kazi bila kupewa taarifa za awali haraka baada ya kwenda kwenye shughuli zake za kila siku za usalama na kufanya kitendo hicho huku akijua ni kinyume na sheria tena akiwa amezungukwa na watu.
Msaidizi mkuu wa kituo hicho Russ Middleton alisema wanaamini hatua hiyo itakua fundisho kwa wengine kutokana na kitendo hicho cha udhalilisha.
Kwa upande mwingine polisi mwingine nchini Uruguay naye alikumbwa na mkasa unaofanana na huo baada ya kucheza na mwanamke akiwa uchi katika kituo chake cha kazi.
Picha ya askari huyo zilinaswa na mitandano mbalimbali na kujikuta zikisambaa kwa kasi hali iliyosababisha ashtakiwe kwa kosa hilo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment