Thursday, February 26, 2015

ATAKA KUUZA FIGO KUKABILIANA NA MASIAHA MAGUMU

Huyu kijana alitaka kuuza figo kutokana na changamoto za maisha,

Hekaheka Feb26
Hali ya maisha imekuwa ngumu kwa kijana huyu Abdallah Omar umri wake ni miaka 17, ana kipaji cha uandishi wa script za movie, akapata nafasi kukutana na Mtangazaji mooja wa habari, ambaye alimkutanisha pia kijana huyu na Zamaradi Mketema ambaye anafanya show inayohusu movie, “Take One” kwenye  TV.
Baadaye kijana huyu alimtafuta tena Mtangazaji na kumuelezea matatizo yake ya kifamilia hali ambayo ilimfanya aamue kuuza figo yake ili aweze kukabiliana na changamoto alizonazo.
Kijana huyo amesimulia kwamba aliwahi kwenda Hospitali ya Amana na kuonana na daktari, baada ya kumueleza nia yake ya kuuza figo daktari alimweleza matatizo ambayo yangeweza kumpata kijana huyo akitoa figo yake kwa umri wake.
Amemuahidi kumsaidia kijana huyo kumkutanisha na watu walio kwenye industry ya movie ili atumie talent yake ya uandishi wa script kupata kipato badala ya kuuza figo.

No comments:

Post a Comment