Thursday, February 19, 2015

WIZI WA WATOTO WAONGEZEKA KENYA

Ishu ya watoto wachanga kupotea Hospitali, kuna hii stori ya waliokamatwa Kenya

weziWanawake wanne wamekamatwa Nakuru Kenya baada ya kudaiwa kuhusika  katika wizi wa watoto wachanga waliotoka kuzaliwa ambapo watoto huzaliwa na kuibiwa kabla ya mama mjamzito kugundua.
Wanawake hao walikamatwa wakiwa na watoto wawili wachanga wenye umri wa siku nne ambao waliwaiba huku mashuhuda wakisema kuwa wizi wa watoto hao unafanyika kwa kushirikiana na mkunga.
Inasemekana wametoka Kisumu yule mama mwingine ambaye tumeshika town ametoka Nairobi na sasa hivi ambapo tunaendelea kuongea unasikia simu  inaitana hapa ni simu ya yule mama ambaye ni mkunga.. kuna simu nyingi ambazo zinapigwa nafikiri wanafanya hiyo biashara ya kununua watoto” alisema askari mmoja baada ya kuwakamata.
Wapo walioshtukia kuwepo biashara hiyo baada ya baadhi ya wanawake kuonekana wakiwa na watoto bila kuwepo dalili yoyote ya ujauzito huku kukiwa na mfululizo wa matukio ya wizi wa watoto ambapo wakunga walihusishwa.

No comments:

Post a Comment