Friday, February 20, 2015

WANANDOA WAMWAGIWA MAJI YA PILIPILI ILI KUTOKA CHOONI

Pale ambapo Polisi wanalazimika kutumia gesi ya pilipili kuwatoa wapenzi chooni..

hopps-court-sex_3203953b
Wapenzi wawili, Lee Hops na Hayley McClory  waliokamatwa wakifanya mapenzi kwenye choo cha pub moja mitaa ya Durman, Uingereza wamepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka ya makosa mbalimbali.
Siku ya tukio mhudumu mmoja  aliwakuta na kutoa taarifa Polisi ambao walitumia gesi ya pilipili ili kuwatoa wawili hao na kuwakamata katika choo cha pub ya Wetherspoons.
25CC500700000578-0-image-a-4_1424274502771
Mlango wa Pub ya Wetherspoons
Wanandoa hao wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kupinga amri ya Polisi, kutoa maneno ya vitisho na matusi na kosa la  kumshambulia Polisi na kuchana koti lake.
Hata hivyo walikana mashtaka hayo huku wakilalamika kwamba sheria ilikiukwa kwa wao kupuliziwa gesi hiyo wakati wa kukamatwa.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia m, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment