Tuesday, February 24, 2015

CAIRO KIBURI

Haya ndiyo maamuzi ya Misri kuhusu michuano ya AFCON 2017…

national-teamWaziri wa michezo nchini Misri, Khaled Abdel-Aziz amesema nchi yake imetupilia mbali jitihada zake za kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2017, na kusema wameamua kujiondoa ingawa wataunga mkono nchi ya Algeria, nchi za Gabon na Ghana nazo ziliomba kuwa wenyeji wa michuano hiyo.
Shirikisho la Soka Barani Afrika linatarajia kutoa jina la wenyeji wa michuano hiyo mwezi April, ambapo Libya nayo ilikuwa miongoni mwa nchi hizo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo, hata hivyo Waziri huyo hakutoa sababu zilizowafanya wajiondoe kwenye kinyanganyiro hicho, huku ikishikilia msimamo huo baada ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA kusema haina maana yoyote kwa nchi mbili za Kiarabu kushindania zabuni hiyo.
Waziri Khaled amesema Misri haitaweza kushindana na Algeria lakini watahakikisha wanatoa msaada kadri wawezavyo, kujiondoa kwa nchi hiyo kumekuja baada vifo vya mashabiki 22, mwezi February wakati Polisi walipokuwa wakipambana na mashabiki kabla ya mchezo kati ya Zamalek na ENPPI, kufuatia tukio hilo shughuli zote za soka nchini humo zimesimamishwa hadi itakapotangazwa tena.

No comments:

Post a Comment