Tuesday, February 24, 2015

BANGI MAREKANI SIO ISHU

Hii kutoka MAREKANI, wao wanaendelea na kuhalalisha matumizi ya bangi…

1375202438_smoking-marijuana-indoors
Kwetu TZ kila siku unakutana na taarifa za watu kukamatwa na bangi, dawa za kulevya, hizi ni kesi ambazo tunazisikia na kuzisoma kila siku kwenye vyombo vya habari, Marekani iko tofauti kidogo mtu wangu.
Alaska linakuwa jimbo la tatu kuhalalisha matumizi ya Bangi ndani ya Marekani, unaruhusiwa kuvuta, kulima na hata ukikutwa na bangi sio ishu kabisa yani kwao.
Kuna baadhi ya viongozi ambao wameanza kuwa na wasiwasi kwamba kama wakati ule wakati bado haijahalalishwa ishu za mauaji na watu kukamatwa kwa makosa ya kufanya vurugu zilikuwa kwa  kiwango cha juu sana, sasa hivi imeshakuwa halali ni nini kitaendelea hasa wakiangalia kwamba kwenye hizo kesi, matumizi ya bangi na pombe yametajwa kuchangia sana.
Bangi ni ruhusa kwa sasa kwenye Jimbo hilo ila marufuku ni moja tu, huruhusiwi kuvuta hadharani, basi.
Majimbo yaliyotangulia kuruhusu hii ni Washington na Colorado, Jamaica nayo imo kwenye list ya nchi zilizoruhusu bangi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot

No comments:

Post a Comment