Thursday, February 26, 2015

CHID BENZ AKWEPA KIFUNGO , MAMA YAKE ALIPA FAINI

 Chid Benz akwepa kifungoChidi-Benz-1

Kwenye story iliyozagaa mjini na mitaani ni  ishu ya  hukumu ya kesi ya rapper Chid Benz ambayo ilikuwa leo, Mahakama ilitoa hukumu kwamba rapper huyo apewe adhabu ya kifungo au alipe fidia.
Chid amelipa faini ya laki 9 na kuachiwa huru ambapo amesema kuwa kesi hiyo imekuwa ni funzo kupitia maisha ambayo ameishi wakati akiwa kwenye kesi hiyo.
Ni watu wawili waliokuwa karibu na Chid wakati wote wa kesi hiyo, mama yake mzazi ambaye ndiye amelipa faini hiyo pamoja na rafiki yake ambaye hakumtaja.
Akiwa anaongea na Soudy Brown, Chid amewapa pole familia ya marehemu Mzee Ebby Sykes pamoja na Mez B kwa kuwa alikuwa mbali na kushindwa kuhudhuria misiba yote miwili.
Hutopitwa na habari na niko tayari kukutumia wakati wowowte kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment