Friday, February 27, 2015

KANYE WEST AMWAGA CHOZI AKIFANYA MAHOJIANO

Kumbukumbu iliyomtoa Kanye West machozi kwenye Interview

rs_560x415-150226132958-1024.Kanye-West-Crying.jl.022615
Story ambazo huwa zinamzungumzia Kanye West mara nyingi zinakuwa za vioja vioja hivi, najua utakumbuka ya kwenye red carpet ambayo aligoma kutabasamu ili apigwe picha.. mara akamwambia msanii Beck kwamba hastahili Tuzo.. mara ikasikika ya kurushiana maneno kati yake na Amber Rose..
Story ya kumuona Kanye West akitoa machozi hii kidogo inaufunua ukurasa mwingine wa rapper huyo, Kanye alikuwa kwenye Interview katika kituo cha BBC Radio 1, kilichomtoa machozi ilikuwa alipomkumbuka rafiki yake aliyefariki, Prof.  Louise Wilson aliyekuwa anajihususha na masuala ya mitindo.
Mtangazaji Zane Lowe na Kanye West
Mtangazaji Zane Lowe na Kanye West
Mara ya mwisho tumekutana kwenye mgahawa ambao napendelea kwenda nikiwa London, mgahawa wa Hakkasan.. ni kama alijua kwamba anakaribia kufariki, akanipa ushauri mzuri wa kunifanya nifanikiwe kwenye maisha.. aliulizia kuhusu mke wangu na mtoto wangu..“– Kanye West.
Wakati akiendelea na interview hiyo machozi yalimtoka, akajifuta halafu akamwambia mtangazaji Zane Lowe ambaye alikuwa akimfanyia Interview hiyo kwamba hakuwahi kutoa machozi akiwa anahojiwa.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitiaww.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment