Wednesday, February 25, 2015

APIGA FAINI DOLA 150 KWA KOSA LA KUHUBIRI BARABARANI

Pale ambapo mahubiri ya mama wa Mchungaji yanawakera wapita njia… Ishu mpaka Mahakamani

prayer26n-1-webMartha Nagbe alijikuta akitozwa faini na Mahakama kwa kesi ya usumbufu na kupigia kelele majirani na wapita njia, lakini ukweli ni kwamba alipigwa faini hiyo kutokana na kufanya mahubiri barabarani kwa sauti ya juu na sio kwamba alikuwa akipiga kelele.
Mke huyo wa mchungaji ambaye amekutana na mkasa huo Dakota, Marekani amepigwa faini hiyo baada ya kukutwa mara kadhaa akihubiri barabarani jirani na makazi ya watu ambao nao waliwahi kulalamika kwamba wanakerwa na kelele za mama huyo, mwisho wa siku Polisi wa doria walimkuta na kumpeleka Mahakamani ambako alipigwa faini ya dola 150 ambazo ni zaidi ya 270,000/- Tshs.
prayer26n-3-web
Mchungaji Juwle Nagbe
Mume wa mwanamke huyo Mchungaji Juwle Nagbe amesema mke wake amesikitishwa sana na maamuzi ya Mahakama hiyo.
Kanisa I
Kanisa la Methodist lililopo Lisbon, Dakota Kaskazini, Marekani ambalo mume wa Martha ni Mchungaji wa kanisa hilo
Mbali na kupigwa faini hiyo Martha amesema hatoacha kusali kwa sababu ana imani na MUNGU na pia anaamini yuko huru kuendelea kufanya mahubiri kwa njia yoyote ambayo ataona iko sawa na imani yake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment