Thursday, February 26, 2015

KOREA NA ISHU YA MICHEPUKO

Korea wameamua hivi kuhusu ishu ya ‘kuchepuka’ kwenye ndoa…

3929-000026
Wakati TZ tunaendesha kampeni ya “Baki njia kuu..michepuko sio dili…epuka UKIMWI” ili kuhimiza watu wajiepushe na mazingira yatakayosababisha kupata maradhi hayo, leo ndio nafahamu kwamba kumbe Korea Kusin walienda hatua nyingine mbele zaidi ya hii, wao walikuwa na Sheria ambayo ilikuwa mtu ukikamatwa yani kwa kesi ya kuchepuka ni kama kesi nyingine tu, unapelekwa Mahakamani na wengi wameshahukumiwa vifungo kabisa.
Ripoti inaonesha toka mwaka 2008 watu zaidi ya 5,500 wamehukumiwa kwa kesi za kuwa na uhusiano nje ya ndoa, jana historia imegeuka kwao, limekaa jopo la Majaji tisa, saba kati yao wamekubali kuwa Sheria hivyo iondolewe.
Jaji  Park Han-Chul alikuwa mmoja ya walioshiriki kwenye jopo hilo, amesema imefika wakati wa kubadili Sheria za masuala ya uhusiano wa kimapenzi kwa watu wao; “Hata kama ishu ya kutoka nje ya ndoa ni kinyume cha maadili ya kijamii, Serikali haipaswi kuingilia masuala ya maisha binafsi ya watu“– Park Han-Chul.
Sheria hiyo ilipitishwa mwaka 1953 ambapo hukumu ilikuwa kama ukikutwa na hatia ya kumsaliti penzi wako kifungo ilikuwa mpaka miaka miwili jela.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment