Friday, February 27, 2015

YALIYONIKUTA TANGA SEHEMU YA (21)



HADITHI

YALIYONIKUTA TANGA (21)

IIPOISHIA TOEO IIOPITA

“Sawa. Leo kamilisha taratibu za kuanza likizo, kesho utaondoka” afande wangu aliniambia.

“Nashukuru afande”

Nikamuaga na kutoka.

Siku ya pili yake nikaanza likizo yangu. Na siku ya tatu nikaondoka kwenda Dar nikiwa nimekichukua kile kisanduku cha dhahabu. Nilikitia kwenye begi langu.

Nilipofika Dar siku iliyofuata nikatafuta usafiri wa kuelekea Kagera. Mpaka ninafika kijijini kwetu ilinichukua siku mbili. Japo nilikuwa nimekutwa na madhila huko Tanga, nilipata furaha kukutana tena na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu ambao tuliachana kwa karibu miaka mitatu iliyopita.

Iliuwa ni siku iliyofuata nilipowakusanya ndugu zangu wawili ambao walikuwa wakubwa zangu pamoja na wazazi wangu na kuwaeleza mkasa uliokuwa umenitokea huko Tanga.

Niliwaeleza wazi makosa ambayo tuliyafanya mimi na Sajenti Erick ya kumbambikia kesi mwanamke ambaye alikuwa ni jini baada ya kukataa kutupa rushwa. Lakini nilijitetea kuwa aliyepanga mpango huo alikuwa mkuu wangu wa kazi ambaye alichinjwa kama kuku.

Pia nilificha kuwaeleza habari ya kile kisanduku cha dhahabu ambacho nilikuwa nimekiiba nyumbani kwa yule mwanamke na ambacho nilikwenda nacho Kagera.

Baada ya kuwaeleza mkasa huo ambao uliwashangaza na kuwatia hofu, wazazi wangu waliniambia ni lazima tutafute mganga tumueleze suala hilo halafu tumsikilize atatuambia nini.

SASA ENDELEA

Baada ya mazungumzo yetu mama alinichukua tukaenda kwa mganga. Mganga mwenyewe alikuwa kijiji cha pili na tulikwenda kwa miguu.

Wakati tunatembea pole pole, mama aliniambia nilifanya vyema kuwahi kurudi kijijini hapo na kuwaeleza mkasa huo kwani kama ningechelewa majini hao wangenichinja kama aivyochinjwa Sajenti Erick.

“Tangu zamani tulikuwa tunasikia sifa za mji wa Tanga, ni mji wenye majini wa hatari. Kumbe wengine wanaishi na binaadamu na wanafanya biashara za dhahabu!” Mama aliniambia.

“IIitokea bahati kwamba likizo yangu ilikuwa ipo tayari, nilicheleweshwa na hayo matatizo tu”

“Bahati yako mwanangu”

Tulipofika kwa mganga nilishangaa kukuta mganga mwenyewe niiyesifiwa kuwa hodari kwa matatizo ya majini alikuwa mwanamke tena akiwa bado msichana.

Hatukukuta watu, tulikuwa ni sisi tu. Baada ya kusalimiana naye alitukaribisha ndani kwani tulimkuta nje ya nyumba yake.

“Tumekuja tuna shida” Mama alianza kumwambia mganga huyo mara tu tulipoingia kweye chumba chake cha uganga kilichokuwa uani mwa nyumba yake.

“Shida gani?” mwanamke huyo akatuuliza.

“Wewe ndiye mtaalamu, tunataka utuambie shida yetu” Mama akamwambia.

“Mimi si mtaalamu, mimi ni mtumishi tu wa wenyewe. Ngojeni niwaite mzungumze nao”

Mwanamke huyo baada ya kutuambia hivyo alichukua upande wa kaniki akajifunika kisha akanusa ugoro. Baada ya kuunusa mara tatu alipiga chafya kisha akatikisa kichwa chake kwa mfululizo.

Wakati anatikisa kichwa alitupa mkono na kutusalimia kwa lugha ya kikwetu ambayo ndiyo iliyokuwa ikitumika zaidi pale kijijini. Lakini wakati ule sauti yake ilikuwa imebadilika na kuwa ya kiume.

Akatuambia kwamba yeye  ndiye mganga mwenyewe na amekuja kusikiliza shida yetu.

“Mimi ni jini wa kiti, mwenye uganga huu. Nataka kusikiliza shida zenu” akatuambia.

“Tunataka ramli” mama akamwambia.

“Oh mnataka ramli…mtapata” akatuambia na kutazama juu ya dari ya miti ya chumba tulichokuwemo.

Aliangalia boriti za ile dari kwa sekunde kadhaa kama aliyekuwa akiangalia kitu kisha akakishusha kichwa chake na kututazama.

“Ramli inakwenda kwa kijana” akatuambia.

“Taire” Mama alitumia neno la kinyumbani lenye maana ya neno hilo taire.

Mwanamke huyo aliinua tena kichwa chake, safari hii hakuchelewa sana akakishusha taratibu.

“Nimeona” akatuambia na kuongeza.

“Nimeona matatizo makubwa sana, yametokea mbali na amekuja nayo hapa”

Mimi na mama tukatazamana.

“Matatizo gani?” Mama akauliza haraka.

Mganga akatazama tena juu.

“Wewe na mwenzako mlifanya makosa, naona damu nyingi…” akatuambia baada ya kukishusha kichwa chake kisha akatazama tena juu.

Iikuwa kama vile pale juu ndipo alipokuwa anasoma habari zetu.

“Mtu mmoja ameuliwa na mmoja amechukua mali, ile mali ni ya majini” mwanamke huyo aliendelea kutuambia.

Tukanyamaza kimya huku tukiendeea kumsikiliza. Niishayatafsiri maneno yake kwamba mtu aliyeuliwa ni Sajenti Erick na aliyechukua mali ni mimi. Mali ilikuwa ile dhahabu iliyokuwemo kwenye kisanduku.

Mwanamke huyo baada ya kutazama juu alishusha kichwa chake na kunitazama mimi.

“Hebu nieleze, nini kimetokea” akaniambia.

Kwa vie aishaigusia habari yenyewe nikaona nimueleze. Nikamueleza.

Mwanamke huyo akapiga mluzi wa mshituko.

“Hatari!” akasema na kuongeza.

“Wewe pia ungekufa. Umri wako bado mrefu”

Akaendelea kutuambia.

“IIe nyumba inakaa majini. Mwenyewe amekwishakufa. Majini wa pwani wanafanya biashara. Wewe unapenda sana kutongoza wasichana. Sasa umetongoza jini. Alikuwa anakutafuta akukomeshe”

Nilimuelewa alichomaanisha. Alikuwa na maana kwamba mimi napenda kutongoza kwa sababu nilimtongoza yule msichana wa kijini kwenye simu, kumbe msichana mwenyewe naye alikuwa ananitafuta baada ya kumkamata mama yake na kumbambikia kesi ya uongo.

“Sasa nifanye nini ili niweze kusalimika” nikamuuiza mwanamke huyo.

Niipomuuliza hivyo alitazama juu. Baadaye aliurudisha chini uso wake akatuambia.

“Wenyewe wanataka dhahabu yao”

“Hakuna namna ya kufanya nikabaki nayo mimi?” nikamuuliza.

“Mimi utanipa nini?”

“Nitakupa pesa utakayoitaka”

“Sawa. Kesho lete kile kisanduku, nitakufanyia uganga wake. Hao majini hawatakufuata tena na wewe utabaki na dhahabu yako”

“Hivyo ndivyo ninavyotaka. Basi tutakuja kesho. Nitakileta na kile kisanduku” nikamwambia.

Yule jini alipoondoka, yule mwanamke alituuliza tulichozungumza, tukamueleza.

“Sasa kesho mtakuja?” akatuuliza.

“Tutakuja kesho asubuhi” nikamjibu.

“Ngoja nikupe dawa yangu” akatuambia na kuinuka.

Aikwenda pembeni mwa chumba hicho. Alikuwa ameweka makorokoro yake ya kiganga. Akachukua pembe moja ya mnyama aliyokuwa ameifunga kitambaa cheusi. Ule upande uliokuwa na shina la ile pembe aliukung’uta kwenye kiganja chake, ukatoka unga mweusi.

Alinifungia unga huo kwenye kikaratasi.

“Usiku utatia dawa hii kwenye maji yako ya kuoga halafu utaoga” akaniambia.

Nikakichuku kile kikaratasi na kukitia mfukoni.

“Niitie yote au niibakishe?” nikamuuliza.

“Tia yote”

“Sawa”

Je nini kitaendelea? Usikose kuendelea na hadithi hii katika toleo lijalo. 
Niko tayari kukutumia habari inayonifia na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

No comments:

Post a Comment