Picha na taarifa ya mtu wa Nicki Minaj aliyeuwawa kwa visu, huyu mwingine kachomwa pia.
Hawa
jamaa wawili wanaoonekana kwenye picha walikua ni sehemu ya timu ya
Nicki Minaj, walikwenda sehemu inaitwa Philadelphia Marekani ambapo ni
siku mbili tu zimepita toka waingie kwenye mji huo kwa ajili kujiandaa
na ziara ya kimuziki ya Nicki Minaj.Polisi wamesema aliyefariki ni De’Von Pickett, 29, au Day Day anaeonekana kushoto kwenye picha Eric Parker, 27 mwingine aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.
Kilichotokea ni wao kuchomwa visu kwenye ugomvi uliotokea wakiwa Baa usiku wa Jumanne na rafiki zao ambapo baada ya kuchomwa visu walikimbizwa Hospitali lakini muda mfupi baadae Day Day akawa amefariki.
Polisi
wamesema watamzawadia milioni zaidi ya thelathini na tano mtu yeyote
atakaefanikisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa aliewachoma visu.
No comments:
Post a Comment