Saturday, May 9, 2015

EBOLA BADO TISHIO

Ebola kwenye headlines kwa mara nyingine tena Marekani !!

IAN CROZIER
Mwaka 2014 stori kubwa kutoka nchi za West Africa zilizokaa sana kwenye vichwa vya habari ni ishu ya ugonjwa wa Ebola.. watu waliofariki ni zaidi ya 5,000, wengine ambao walipata maambuizi ya ugonjwa huo ni zaidi ya watu 10,000… changamoto kubwa ilikuwa kupatikana kwa dawa na chanjo ya kuzuia ugonjwa huo.
Ian Crozier alikua ni mmoja wa madaktari waliojitolea kwenda Sierra Leone kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola.. muda wake ulipoisha alirudi nyumbani kwao, Atlanta Marekani ambako waligundua kuwa ana maambukizi ya Ebola, akawekwa kitengo maalum kwa ajili ya matibabu.
IAAN 2
Miezi michache imepita toka Dr. Crozier atibiwe, stori kwenye headlines leo inamhusu tena yeye.. amegundulika kuwa na kirusi cha Ebola kwenye jicho la kushoto.
Utafiti unaonesha Dr. Crozier hawezi kumuambukiza mtu yoyote kirusi hicho, tofauti na ilivyozoeleka kwamba mtu mwingine akigusana na mgonjwa anapata maambukizi pia.
Uchunguzi bado unaendelea japo inaonekana kama Dr. Crozier asipopatiwa matibabu mapema huenda akapata tatizo la upofu.
Dr. Crozier ni mgonjwa wa kwanza kuugua Ebola mara mbili mfululizo.

Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukusogezea muda wowowte kupitia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment