MAPINDUZI YAFELI BURUNDI
Mnamo 13 mwezi May
jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa
Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini
msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi
mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.


Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
1-Majenerali waasi kushtakiwa

No comments:
Post a Comment