Mnamo 13 mwezi May
jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa
Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini
msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi
mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.Rais Nkurunziza alidaiwa
kurudi nchini Burundi kutoka Tanzania ,lakini imethibitishwa ,
alishindwa kufanya hivyo na kwamba yungali nchini Tanzania.
21.15pm:-Nkurunziza hayuko Tanzania,Je Yuko wapi?
Rais Nkurunziza
Msemaji wa rais Nkurunziza
Willy Nyamitwe amezungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwa
Nkurunziza aliondoka nchini Tanzania siku ya jumatano lakini hawezi
kubaini iwapo yuko nchini Burundi au la.Amesema kuwa kutokana na maswala
ya usalama hawezi kutaja mahala alipo lakini yu buheri wa afya.
20.28pm-Wanajeshi watiifu wa Nkurunziza
Mji wa Bujumbura
Wanajeshi walio watiifu kwa
rais Pierre Nkurunziza wametangaza kudhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu
wa Bujumbura siku moja baada ya jaribio la mapinduzi.Kulikuwa na
mapigano makali mjini Bujumbura,hususan katika kituo cha habari cha
kitaifa,lakini makabiliano hayo yameisha huku wanajeshi watano wakidaiwa
kuuawa.
18.05pm-Wanajeshi watiifu
Wanajeshi watiifu wapiga doria Bujumbura
Makundi hasimu ya jeshi la
Burundi yamekuwa yakipambana kukidhibiti chombo cha kitaifa cha habari
RTBN ambacho kilizimwa kwa mda .Duru zimearifu kuwa kituo hicho cha
habari kiko chini ya udhibiti wa vikosi vinavyomtii rais Pierre
Nkurunziza.
17.53pm-Viongozi wajadili Burundi
Baraza la usalama la umoja wa Afrika laijadili Burundi kwa sasa
Baraza la usalama la umoja wa
Afrika limetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter likisema kuwa
wanachama wa baraza hilo kwa sasa wanaijadili.
17.00pm-Wanajeshi wapiga doria
Maafisa wa polisi wapiga doria Burundi
Maafisa wa polisi waliojihami katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wanaonekana wakilinda vizuizi vya barabarani leo
16.50pm-Mkutano kuhusu Burundi waendelea.
Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Afrika
Baraza la usalama la umoja wa Afrika kwa sasa linaijadili Burundi.
tweets: "Chini ya Uongozi wa balozi Amina Diallo wa Niger,ni mkutano wa 507.Baraza hilo linaangazia hali ilivyo Burundi
16.10pm-RNTB yarudisha matangazo
Kituo cha redio
Kituo cha redio cha Burundi
RNTB kimerudi hewani,chini ya wanajeshi walio watiifu kwa rais Pierre
Nkurunziza kulingana na duru kutoka kwa wanajeshi.Tumethibitisha kuwa
kimeanza kurusha tena matangazo.
15.50pm-Nkurunziza asema yuko tayari kusamehe
Ris wa Burundi Pierre Nkurunziza
Shirika la habari la Reuters
limenukuu baadhi ya mahojiano yaliofanywa na rais Nkurunziza na kituo
cha habari cha RTNB mapema jana.
''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi'',alinukuliwa akisema.
''Nawashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.
Lakini baada ya mahojiano hayo kulikuwa na vita karibu na kituo hicho cha habari ambacho kwa sasa kimezimwa. 15.47pm-Ramani ya Burundi Kituo cha habari cha Burundi
Isanganiro kimesema kuwa kimefungwa na vituo vyengine vya kibinafsi
.Kituo hicho ni miongoni mwa vile vilivyotangaza mapinduzi siku ya
jumatano.
15.17pm-Kituo cha habari
Askari Burundi
Kituo cha habari cha Redio ya RTNB kimezimwa kufuatia mapigano makali karibu na afisi zake mjini Bujumbura.
15.01pm:Rais wa Burundi Ahojiwa
Wanajeshi nchini Burundi wakipiga doria
Kituo cha habari cha Burundi
RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.Vita
vimezuka karibu na afisi za kituo hicho cha habari.Jenerali anayeunga
mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP
kwamba vitengo vinavyopigana kumpindua vimepata agizo la kukiteka kituo
hicho habari cha RTNB kwa kuwa wana uwezo.
14.30pm:Makundi ya vijana waliojihami
Vijana Burundi
Kuna madai kwamba kundi la
vijana linalunga mkono serikali limeshambulia kituo kimoja cha habari
cha kibinafsi mjini Bujumbura.KUndi hilo linalojulikana kama
Imbonerakure,baadhi ya watu wanaamini kwamba vijana hao wanatumiwa kama
wapiganaji na kwamba huenda wamepewa silaha ili kuwatishia raia kabla ya
uchaguzi.
13.45pm-Hali ni tete Burundi
Wanajeshi wa Burundi
Hali bado ni tete nchini
Burundi siku moja tu baada ya jenerali mmoja wa jeshi kujaribu
kutekeleza mapinduzi .Barabara nyingi zimeendelea kuwa bila watu kwa
kipindi kirefu cha alfajiri huku wengi wakisalia ndani ya majumba yao
wakihofia usalama kulingana na mwanahabari wetu Ruth Nesoba.
13:30pm-Ukabila
Kiongozi wa jeshi aliyetangaza mapinduzi
Tofauti zilizopo katika jeshi
la Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi hazionekani kuwa katika misingi
ya kikabila ,mkuu wa majeshi ambaye ni mtiifu kwa rais Nkurunziza
pamoja na jenerali wa majeshi aliyetangaza mapinduzi hayo ni wa kabila
la Hutu.Makundi hayo yanaonekana kugawanyika kati ya wale wanaoamini
rais Nkurunziza alikiuka makubaliano ya amani yaliomaliza vita vya
wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka kuongoza kwa muhula wa tatu na wale
wanaosalia kuwa watiifu kwake
12:05pm-Wanajeshi watiifu
Mj wa Burundi Bujumbura
Afisa mmoja wa kijeshi
ameiambia BBC Afrique kwamba wanajeshi watiifu nchini Burundi
wanadhibiti mji wa Bujumbura ,uwanja wa ndege,makao ya rais pamoja na
vituo vya redio na runinga.
12:00pm-Milio ya Risasi
Wanajeshi wa Burundi
Makundi hasimu ya askari
yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala
ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza,
amepinduliwa.
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
Ungana nami kwa matukio kemekem na kujua kinachojiri pale Bunjubura ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment