Friday, May 15, 2015

MUUGUZI AINGIA MATATANI

Muuguzi kwenye tuhuma za kumtesa mtoto!!

legs
Unyanyasaji wa watoto umeendelea kuwa sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakikithiri sana ndani ya familia na jamii za watu wengi duniani.
Kitendo cha msichana wa kazi kule Uganda kumtesa mtoto wa bosi wake  kwa kumpiga bado hakijasahaulika na mamilioni ya watu duniani baada ya kunaswa na kamera na kusambazwa kwenye mitandano ya kijamii.
Tukio la aina kama hiyo limetokea tena kule Bulgaria baada ya muuguzi Emiliya Kovacheva kumtesa kwa kumpiga mtoto mchanga wa siku nne bila kuwa na huruma kwa madai anapiga kelele.
Mtoto huyo Nicole aliyekuwa ameachwa na mama yake alipata majeraha makubwa kufuatia mateso kutoka kwa muuguzi huyo.
Awali muuguzi huyo alikataa kuwa amefanya kosa hilo lakini baadaye alikiri baada ya kuonyeshwa video baada ya kamera kunasa tukio zima ndani ya chumba hicho cha hospitali na kusema alifanya hivyo kutokana na kuchanganyikiwa baada ya mtoto huyo kukataa kulala na kuwasumbua watoto wengine waliokuwa wamelala.
Kwa sasa muuguzi huyo anakabiliwa na kosa la mauaji

No comments:

Post a Comment