Wednesday, May 20, 2015

QATAR YATAKIWA KUBADILIKA

Boresheni hali ya wafanyakazi :Amnesty

Maandalizi ya kombe la Dunia
Shirika la Haki za binadamu la Amnesty International ,linasema Qatar inalazimika kuboresha hali ya wafanyakazi wahamiaji wakati huu nchi hiyo inapoendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia mwaka 2022.
Amnesty wanasema Qatar imepiga hatua kidogo sana kutekeleza ahadi nyingi walizozitoa mwaka jana, kwani wafanyakazi bado wanahitaji ruhusa kutoka kwa waajiri wao ,kubadili ajira au kuondoka nchini humo,mabadiliko ya malipo kwa wafanyakazi yanafanyika taratibu mno wakati ni jambo la muhimu mno.
Hata hivyo Serikali ya Qatar inasema mabadiliko makubwa yanakuja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu,japo kuwa Amnesty inaitaka FIFA , kuishinikiza Qatar kuongeza kasi katika kuleta mabadiliko.

No comments:

Post a Comment