Tuesday, May 19, 2015

RAHEEM STERLING KUTIMKIA ARSENAL

Msimamo wa Sterling kwa klabu yake ya Liverpool huu hapa…

 liverpool
Klabu ya Liverpool imepanga kuwa na mazungumzo mazito na winga wake, Raheem Sterling wiki hii baada ya mchezaji huyo kumtamkia kocha Brendan Rodgers kuwa anataka kuondoka.Sterling alifanya maungumzo binafsi na kocha wake Rodgers kabla ya mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea na akaweka wazi hataki kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Lakini akakubali kukutana na klabu kwa mazungumzo ya mwisho kabla ya kufanya uamuzi rasmi wa kubaki, au kuondoka ndani ya klabu hiyo.
Sterling amegoma kusaini Mkataba mpya wa miaka mitano kwa sababu haridhishwi na uwezo wa timu kiushindani, kwani kiu yake ni kucheza Ligi ya Mabingwa na kushinda mataji.
Aidha, mshahara wa Pauni 90,000 kwa wiki anaolipwa sasa haumridhishi, ingawa klabu imeahidi kumpandishia hadi pauni 100,000 katika mkataba mpya.
Vigogo wa Ligi Kuu England  Chelsea, Manchester City, Arsenal na Manchester United wanamtaka mchezaji huyo kinda  na wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu.
Unahitaji

No comments:

Post a Comment