Saturday, May 16, 2015

SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MAY 16 TZ

Uchambuzi huu kutoka magazetini unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kipo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

What The Papers Say
MWANANCHI
Wakati Mkutano wa Bunge ukianza kwa mjadala wa uliopoteza mwelekeo na kutawaliwa na malumbano kati ya Wabunge wa CCM na wa Vyama vya Upinzani, Naibu Spika Job Ndugai amesema ni vigumu hali hiyo kuzuilika kwa kuwa mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi.
Bunge hilo lilipokea na kuanza kujadili Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo yaliibuka malumbano ya kisiasa huku Wabunge wa Upinzani wakilalamikia udhaifu wa Serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa miaka 10 iliyopita.
Mwaka huu ni wa Uchaguzi huwezi kuzuia hiyo hali na kumbuka kuwa Wabunge ni Wanasiasa.. Wabunge homa zipo juu na hawawezi kukaa hapa wakati katika Majimbo yao wanapigiwa simu kuwa yamevamiwa”—Naibu Spika Job Ndugai.
Baadhi ya Wabunge walisema agenda kuu kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu kwa kuwa hiki ni kikao cha mwisho cha Bunge na baada ya hapo wote wanarudi Majimboni kwa ajili ya Uchaguzi.
MWANANCHI
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imewabana walimu wa Shule ya Sekondari ya Msimbu na kuwataka waandike barua kujieleza baada ya kushika nafasi ya mwisho Kiwilaya katika matokeo ya Kidato cha Pili na kidato cha nne 2014.
Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Mwamvua Mrindoko alisema waliunda Kamati kuchunguza sababu ya kufeli huko.
Mrindoko amesema  baadhi ya sababu walizobaini kuchangia kufeli kwa wanafunzi wengi iko ya ushirikiano duni kati ya shule na Jamii, msukumo mdogo wa wazazi kwenye elimu pamoja na utoro wa wanafunzi.
NIPASHE
Kutokana na machafuko yanayoendelea Burundi na kusababisha kufurika kwa waomba hifadhi mkoa wa Kigoma, kambi ya Nyarugusu imejaa na kusababisha shule zilizopo ndani ya kambi hiyo kufungwa kwa muda.
Kwa kawaida kambi hii ina uwezo wa watu 50,000 kulingana na taratibu za kimataifa, lakini mpaka sasa ina wakimbizi 54,706…hivyo baada ya kuanza kuwapokea waomba hifadhi wapya Aprili 29, mwaka huu, tumepata wapya 16,808 hadi juzi”– alisema Mkuu wa kambi hiyo, Sospeter Boyo.
Alisema kwa sasa wamefunga shule ili majengo hayo yatumike kuwahifadhi wahamiaji wapya wanaowasili kila siku huku wakifanya jitihada kupata sehemu nyingine ya kuwahifadhi.
Baadhi ya wakimbizi kambini hapo, walisema kitendo cha kushindwa kuondolewa madarakani kwa Rais Pierre Nkurunzinza, kimewasikitisha kwani kitasababisha kuwapo na machafuko zaidi.
Tunasikitika sana kwa jaribio hilo kutofanikiwa, sasa hali itakuwa mbaya zaidi nchini kwetu kutokana na machafuko ya kushindwa kuondolewa madarakani Nkurunzinza”– alisema mmoja wa wakimbizi hao.
Wakimbizi hao wamesema Demokrasia ndani ya Burundi imepotea na pia kunafanyika mauaji ya kimya kimya kwa wananchi wenye mlengo tofauti na Rais aliyepo madarakani.
NIPASHE
Mbunge Suleiman Said Bungara ‘Bwege’ ametofautiana na wabunge wenzake wa upinzani wanaosema Serikali ya CCM imechoka, badala yake amesema Watanzania ndio waliochoka huku akisema kuwa wapo wabunge wanaoitetea serikali kwa kuibeba, lakini wapo wabunge wanaofanya kazi zao za kuikosoa.
Bwege alisema serikali haijachoka kama wengine wanavyosema isipokuwa waliochoka ni Watanzania wanaoibeba serikali hiyo wamechoka, wamejiandaa kuiondoa madarakani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na kuwaweka wagombea wa UKAWA madarakani.
Fungeni virago muondoke… anakuja Mbunge hapa na kusema serikali imejenga shule, Zahanati halafu baadaye wanaomba/wanalalamika miradi ya maendeleo katika majimbo yao haijatekelezwa.. Wabunge wa CCM wamechoka, wanajiaga wenyewe”—Suleiman Bwege.
Hoja ya kuchoka kwa Serikali ya CCM ilitolewa na Mbunge Tundu Lissu akiituhumu serikali hiyo kwa kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.
Tangu siku hiyo wabunge wengi wa upinzani wanaochangia hotuba ya Waziri Mkuu wamekuwa wakitumia lugha hiyo huku Wabunge wa CCM wakijitutumua kuitetea kuwa haijachoka.
Kila siku asubu na mapema tangakumekuchablog inakupatia kurasa za magazeti mwanzo mwisho na kufuatiwa na uchambuzi wa habari muhimu katika magazeti yote, usiwe mbali nami ni hapa hapa 

No comments:

Post a Comment