Saturday, May 16, 2015

VATICAN KULITAMBUA TAIFA LA PALESTINA

Papa Francis akutana na rais wa Palestine

Papa Francis akutana na rais wa Palestine
Kiongozi wa Wakatoliki duniani Papa Francis amefanya mazungumzo na rais wa Palestina Mahmoud Abbas huko Vatican.
Papa Francis alimmiminia sifa Abbas akimtaja kuwa, kuwa ni malaika wa amani.
Kiongozi huyo wa wakatoliki alimsifu Abbas kabla ya kumtunukia medali ya amani.
Ziara ya bwana Abbas inawadia siku chache tu baada ya utawala wa kanisa Katoliki duniani wenye makao yake huko Vatican kutangaza kuwa wataweka sahihi ya kwanza na wapalestina hivi karibuni.
Mkataba huo utakaotiwa sahihi karibuni unatambua hoja ya kuweko kwa mataifa mawili mkabala ilikuchochea amani baina ya wapalestina na waisraeli.
Kulingana na Vatican hiyo itahakikisha kutambuliwa kwa wakatoliki katika maeneo yanayotawaliwa na rais Abbas.
Israeli kwa upande wake ilitangaza kutofurahishwa kamwe kwa mkataba huo baina ya kanisa katoliki na taifa la Plaestina kwani inatambua ''Palestina kuwa taifa''
Rais Abbas yuko Vatican kuhudhuria kutawazwa kwa watawa wa kipalestina na kanisa katoliki.
Sherehe hiyo itafanyika hapo kesho.

No comments:

Post a Comment