Thursday, May 7, 2015

VYOMBO VYA HABARI UJERUMANI VYAMBEBESHA LAWAMA PEP GUARDIOLA

Magazeti ya Ujerumani yamponda Pep Guardiola.

HERZOGENAURACH, GERMANY - AUGUST 13:  Pep Guardiola, head coach of FC Bayern Muenchen visits the Adidas headquarter on August 13, 2013 in Herzogenaurach, Germany.  (Photo by Lennart Preiss/Getty Images For Adidas) *** Local Caption *** Pep Guardiola
HERZOGENAURACH, GERMANY – AUGUST 13: Pep Guardiola, head coach of FC Bayern Muenchen visits the Adidas headquarter on August 13, 2013 in Herzogenaurach, Germany. (Photo by Lennart Preiss/Getty Images For Adidas) *** Local Caption *** Pep Guardiola

Ikiwa imepita siku moja tangu Bayern Munich ilipofungwa na Barcelona kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa , kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amejikuta akibebeshwa lawama za kipigo hicho na magazeti ya kila siku ya nchini Ujerumani .
Gazeti la Bild liliandika kuwa ‘Guardiola amefungwa na Barcelona na hakukuwa na muda wa kumbukumbu nzuri ya kurudi kwake nyumbani kwao Barcelona’ huku likiendelea na mlolongo wa lawama kwa kocha huyo kwa kusema kuwa ‘Barca ilimuonyesha kocha huyo udhaifu alio nao’.
Gazeti hilo lilikumbusha kuwa kipigo cha 3-0 ambacho Bayern ilikipata ni kipigo kibaya kuliko vyote alivyowahi kupata akiwa na Bayern sambamba na kipigo kingine cha 3-0 dhidi ya Borrusia Dortmund , 4-0 dhidi ya Real Madrid  na 4-1 dhidi ya VFL Wolfsburg , huku likimaliza kwa kuuliza kama ataweza kugeuza kipigo hiki .
Gazeti lingine la kila siku la Die Zeit liliandika kuwa Bayern na Pep Guardiola kwa pamoja wamepewa darasa la jinsi ya kucheza soka katika mchezo wa jana .
Gazeti la kicker limekwenda mbali zaidi kwa kuandika kuwa hiki kilikuwa zaidi ya kipigo na kwamba matokeo hayo yamemuacha Guardiola akiwa amepigwa butwaa .
Wachezaji wengi wa zamani nchini Ujerumani walilalamikia mbinu zilizotumiwa na Pep Guardiola kwenye mchezo huo, akiwemo kipa wa zamani Oliver Kahn ambaye alilaumu jinsi ambavyo Bayern ilishindwa kujilinda na kuizuia Barcelona isifunge .
Katika mchezo wa juzi Bayern Munich ilifungwa 3-0 baada ya Lionel Messi kufunga mabao mawili na kutengeneza bao lingine lililofungwa na Neymar na kuiacha Bayern Munich ikiwa hatarini kutolewa kwenye nusu fainali kwa msimu wa pili mfululizo .

No comments:

Post a Comment