Monday, May 11, 2015

WATOTO WASAFIRI NA KUJIFICHA KWENYE CHESESS

Hii ishu ya watoto kusafiri kwenye chasis ya basi ni moja ya stori kubwa leo May 11 2015

Singida KIds
Moja ya story kubwa kuripotiwa na kituo cha ITV jana jioni  ni ishu ya watoto watatu wa kiume kukutwa wakiwa wamejificha kwenye chasis ya basi.
Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.
Watoto hao wamesema walitolewa na mtu mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia kuna kazi, walipofika Kahama akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa njia hiyo ya kujificha kwenye chasis ya basi.
Kamanda wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo la Mgamba Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya Kilometa 360.

No comments:

Post a Comment