Neymar kaingia kwenye matatizo tena na Serikali ya Brazil, safari hii na gari lake limekamatwa..
Staa wa Soka, mkali mwingine toka Brazil ambaye anachezea Klabu ya Barcelona
hii sio taarifa nzuri kwake, wafatiliaji wa mambo wanasema inafanana
kabisa na ishu ambayo aliwahi kuhusishwa nayo pia ya kukwepa kulipa Kodi
ya Serikali mwaka 2013 alipokuwa anahama kutoka Klabu ya Santos kwenda Barcelona.
Kingine kinachomhusu Neymar nyumbani kwao Brazil ni kwamba, Idara ya Serikali ya Brazil inayohusika na ukusanyaji wa Mapato imelikamata gari lake aina ya Porsche na kesi inayohusu gari hilo ni kwamba inadaiwa Neymar
alikiuka Sheria wakati anaanza kulimiliki gari hilo, na mpaka hatua za
mwisho wakati gari linaingizwa Brazil na linatua mikononi mwa Neymar mwenyewe kuna kanuni za masuala ya mapato zilikiukwa !!
Taarifa zilizogusa Vyombo vya Habari kuhusu ishu hiyo zinasema Neymar na baba yake walishinda gari hilo kwenye mchezo wa bahati nasibu baada ya Neymar kuwa mfungaji Mwaka bora Mwaka 2011 kwenye Michuano ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Mpaka sasahivi gari linashikiliwa na
Serikali na wamesema halitoachiwa mpaka Kesi yake na watu wa Mamlaka ya
Mapato iishe… Hii inakuwa mara ya pili kwa Neymar kuhusishwa na ishu ya kukwepa kulipa Kodi nyumbani kwao Brazil.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment