Takataka zikiwa zimezagaa hadi barabarani barabara ya 11
Ngamiani Tanga na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa njia hiyo na
wafanyabiashara wenye maduka jirani na uchafu huo.
Takataka hizo ziko katikati ya jiji la Tanga maeneo ya Ngamiani ambapo ndipo kitovu kikuu cha biashara na wageni waingia na watokao.
Baadhi ya watu wakiwemo wafanyabiashara na wenye maduka wameiambia Tovuti ya Tangakumekuchablog kuwa hali hiyo inatisha na hivyo kutaka mamlaka inayoshughulika na usafi kufanya jitihada za kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi na kuondokana na fedheha ya Tanga kuwa jiji.
No comments:
Post a Comment