Bikizee wa miaka 94 arejea kazini Marekani
Mama mmoja
Mmarekani mwenye umri wa miaka 94 amerudi kazini kama askari waitwao
Park Pangers wa kuhuduma katika mbuga na hifadhi za kitaifa nchini
Marekani.
Bi Betty Reid Soskin, alikuwa ameacha kazi baada ya mkasa kumkumba ulimfanya.Katika mkasa huo mwizi alimvamia nyumbani kwake tarehe 27 Juni, akamgonga ngumi kichwani na kumwibia simu, tarakilishi, vito vya thamani na hata medali yake aliyokuwa ametunukiwa na rais Obama.
Lakini anasema alitaka sana kurejelea maisha aliyoyazoea.
Bi Soskin, alikuwa mwelekezi katika hifadhi ya kihistoria iliyoko eneo la San Francisco Bay kwa muda wa miaka 10.
Aliporudi amepokelewa kwa furaha na wafanyikazi mwenzake wa zamani na anasema ana hamu ya kurudi katika shughuli alizozizoea katika hifadhi hiyo kabla ya kustaafu.
Akiwashukuru wenzake waliompokea vyema, alitania kwamba ilibidi asubiri hadi majeraha aliyopata usoni kwenye mkasa huo wa kuibiwa, yapone ndipo akanyage ofisini hapo kwa kuhofia kuwa angepigwa picha ambazo zingesambazwa katika mitandao kama vile ya YouTube.
Wizara ya maswala ya ndani ya Marekani wameahidi kumpa medali nyengine Bi Soskin kufidia hiyo iliyokuwa imeibwa.
Bi Soskin pia aliwahi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Obama ambako alionekana akikumbatia picha ya nyanyake ambaye alitoka katika kizazi cha ukoo wa watumwa.
Bi Soskin pia ni mwanablogu anaendika sana kuhusu historia ya familia na maisha yake binafsi tangu akiwa karani kwenye meli za enzi za vita vikuu vya dunia.
Kama anavyoonekana katika picha hizo za makaribisho ya wafanyikazi wenzake hapo hifadhi ya Rosie the Riveter World War Two Home Front National Historical Park ni vigumu kukadiria umri wake.
BBC
No comments:
Post a Comment