Makondawa daladala ifanyayo safari yake kati ya Tanga mjini na Pongwe Tanga wakibadilisha tairi barabara ya Korogwe Road eneo la Maziwa na kutoweka alama ya usalama barabarani jambo ambalo linaweza kuhatarisha ajali na usalama wao.
Hali hii imekuwa ya mazoea itokeapo hitilafu ya magari baada ya madereva kutokuwa na alama za barabarani kwenye magari yao na kusababisha ajali ya kujitakia.
Ni hivi karibuni Kikosi cha Usalama barabarani kilikuwa kikifanya ukaguzi magari ambayo hayana alama za barabarani na kuweza kutoa somo kwa madereva wengi ila kuna baadhi hawajui wajibu wao kama ilivyoelezwa na Shaib Ally mkazi wa Mikanjuni Tanga.
No comments:
Post a Comment