Mbunge wa EAC Hafsa Mossi auawa Burundi
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki
katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara
ya Gihosha, eneo la Nyankoni.Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Msemaji wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe amesema amesikitishwa sana na mauaji ya mwanasiasa huyo.
Waziri wa mambo ya nje Alain Aime Nyamitwe pia ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji hayo.
“Nimehuzunishwa sana na mauaji ya leo#Bujumburaya Mheshimiwa Hafsa Mossi, na mwanachama wa#EALA. Ni hasara kuu kwa taifa na#EAC,” ameandika kwenye Twitter.
No comments:
Post a Comment